BENO NJOVU (KULIA) AKIWA NA MWENYEKITI WAKE, YUSUF MANJI |
Kauli hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa
Yanga, Benno Njovu inakinzana na taarifa ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi, aliyeahidi kuzikalisha chini pande zote (Yanga na Azam
TV) ili kutatua utata uliopo kwa ajili ya Azam TV kuonyesha mechi zao.
Tayari Azam TV imeingia mkataba na Bodi
ya Ligi na TFF kwa ajili ya kurusha mechi za ligi huku kila klabu ikinufaika na
kitita cha Sh milioni 100. Hata hivyo, ni Yanga pekee iliyogomea kiasi hicho
kwa madai kuwa ni kidogo kwao.
Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu, amesema
hawana mpango huo wa kuketi chini na msimamo wao ni uleule.
“Yanga haijawahi na haina mpango wa
kukaa chini kuzungumza na hao Azam TV kujadili suala hilo. Taarifa za awali
kila mmoja anazijua na msimamo wetu ni uleule,” alisema Njovu.
Katika mkutano mkuu wa klabu hiyo
uliofanyika Januari 19, mwaka huu kwenye Ukumbi wa PTA, Dar, Mwenyekiti wa
Yanga, Yusuf Manji, aliapa kuwa kiasi hicho hakiwezi kukubalika na kuiomba bodi
ya udhamini chini ya Francis Kifukwe kusimamia vilivyo haki yao kwa kupinga
kiasi hicho.
Njovu amesema wanachotaka kusikia ni
Azam TV kuwaongeza mkwanja, hadi ufikie ule unaoendana na hadhi ya Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment