Mwamuzi
aliyempiga kadi nyekundu Cristiano Ronaldo katika mechi kati ya Real Madrid dhidi ya Athletic Bilbao iliyomalizika
kwa sare amesimamishwa kwa mwezi mmoja.
Pamoja
na kusimamishwa huko, Miguel Angel Ayza Gamez hatachezesha mechi yoyote ya Real
Madrid msimu huu.
Kamati
ya Ligi ya waamuzi wa Hispania (CTA) imemsimamishja mwamuzi huyo kutokana na
kutokuwa makini.
Taarifa
kutoka Hispania zinasema nusura Gamez aondolewe kabisa katika kuchezesha La
Liga msimu huu kutokana na kushindwa kabisa kuuthibiti mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment