Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameondoka leo (Februari 17 mwaka huu) kwenye
Cairo, Misri kujitambulisha kwa uongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF).
Akiwa Cairo, Rais Malinzi ambaye
alichaguliwa Oktoba 28 mwaka jana atakutana na Rais wa CAF, Issa Hayatou pamoja
na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Hicham El Amrani.
Akiwa mjini Cairo, Malinzi atapata
nafasi ya kukutana na viongozi hao lakini pia kutembelea ofisi za makao makuu
ya Caf. Pia atakutana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa shirikisho hilo kubwa
zaidi barani Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment