Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewalalamikia
wanafamilia watano wa mpira wa miguu kwa Kamati ya Maadili kuhusiana na
udanganyifu katika mtihani wa utimamu wa miili ya waamuzi, lakini pia kuhusiana
na suala la usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi.
Riziki Majala na Army Sentimea ambao
ni wakufunzi wa waamuzi, na Oden Mbaga na Samwel Mpenzu ambao ni waamuzi
wanadaiwa kugushi nyaraka kuhalalisha mtihani huo kinyume cha taratibu.
Naye, Sabri Mtulla analalamikiwa ambaye
ni mmoja wa maofisa wa shirikisho hilo, TFF inalala kwa madai ya kuidanganya
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi lolote juu ya
usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli.
Okwi alisajiliwa na Yanga akitokea SC
Villa ya Uganda, wakati huo pia usajili wake ulikuwa bado una utata kuhusiana
na suala la kesi yake na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia iliyokuwa
imemsajili kutokea Simba.
Baadaye TFF ilisimamisha usajili wake
hadi na kutaka ufafanuzi wa uhalali wake kutokea kwa Shikirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa).
Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko hayo
yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo itachunguza ili kujiridhisha kama
yana msingi au la. Ikibaini kuna kesi ndipo walalamikiwa watafika mbele ya
kamati hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment