Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) imeagiza kifanyike kikao cha dharura kati ya
Sekretarieti ya TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na benki ya CRDB ili
kutathimini maendeleo ya matumizi ya tiketi za elektroniki.
Lengo la kikao hicho ni kutathimini
maendeleo ya utekelezaji wa mfumo huo wa tiketi za elektroniki ni kutafuta
ufumbuzi pamoja changamoto zake.
Viwanja vinane nchini vimefungwa
mfumo huo wa tiketi za elektroniki. Viwanja hivyo ni Uwanja wa Azam uliopo
Chamazi, Uwanja wa Kaitaba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid,
Uwanja wa Mkwakwani, na CCM Kirumba.
0 COMMENTS:
Post a Comment