TARIMBA |
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya uteuzi wa wajumbe kuunda kamati mbili za
awali za haki, na kamati mbili za rufani za vyombo hivyo.
Rais wa zamani wa Yanga, Tarimba
Abbas ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ataongoza Kamati ya Nidhamu. Wajumbe
wanaounda kamati hiyo ni Wakili Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti), Kassim Dau,
Nassoro Duduma na Kitwana Manara.
Kamati ya Rufani ya Nidhamu
inaendelea kuongozwa na Profesa Mgongo Fimbo wakati makamu wake ni Wakili
Hamidu Mbwezeleni. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Titus Bandawe, Twaha
Mtengera na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio
ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria anaongoza Kamati ya Maadili. Wajumbe ni
Wakili Ezekiel Maganja, Wakili Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Said Mtanda.
Kamati ya Rufani ya Maadili inaundwa
na Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu
Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.
0 COMMENTS:
Post a Comment