MAREHEMU CHANGA, WA TATU KUTOKA KUSHOTO MSTARI WA NYUMA AKIWA NA KIKOSI CHA JKT RUVU WAKATI WA UHAI WAKE |
Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa
mchezaji wa Vijana, Moro United na Yanga, Omari Changa kilichotokea juzi
(Februari 1 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Msiba huo ni
mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Changa wakati wake uwanjani
akichezea timu mbalimbali alitoa mchango mkubwa ambao tutaukumbuka daima.
TFF tunatoa
pole kwa familia ya marehemu Changa, klabu ya Moro United na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Katika maziko
TFF itawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Kidao Wilfred, na imetoa
rambirambi ya sh. 200,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment