Shabiki mmoja anashikiliwa na Jeshi
la Polisi akidaiwa kukutwa na tiketi bandia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) kati ya Yanga na Simba iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Matei Cosmas (28) ambaye ni mkazi wa
Buza Njiapanda Kitunda, Dar es Salaam amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014
kwenye Kituo cha Polisi Chang’ombe akidaiwa kupatikana na tiketi bandia.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) leo asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia Kituo cha Polisi Chang’ombe
kusaini hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa.
Ni imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa
atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchini.
Tunatoa mwito kwa washabiki wa mpira
wa miguu kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi mwa watu, kwani kufanya hivyo
ni kosa. Tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu zenye chapa ya TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment