Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga
Stars) inaendelea kujinoa kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza
ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia (Shepolopolo)
itakayochezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka huu).
Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian
Kaijage na Msaidizi wake Nasra Juma inaendelea vizuri, na kwa mujibu wa programu
ya benchi lao la ufundi kesho (Jumatatu), Jumanne na Jumatano itafanya mazoezi
saa 10 jioni.
Mazoezi hayo yatafanyika Uwanja wa
Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Uwanja huo
ndiyo utakaotumika kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Shepolopolo ambayo ilishinda mechi ya
kwanza mabao 2-1 wiki iliyopita inatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi (Februari
27 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet, na siku hiyo hiyo itafanya mazoezi Azam
Complex.
Waamuzi wa mechi hiyo Ines Niyonsaba,
Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis Iratunga, wote kutoka Burundi
wanatarajiwa kuwasili nchini Jumatano
0 COMMENTS:
Post a Comment