Pamoja na kuwa na sifa ya kuwahi kuwapa wakati mgumu Al Ahly ya Misri, wakati huo akiinoa Berekum Chelsea ya Ghana, Kocha Mkuu
wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amesema Waarabu hao si kazi ndogo.
Kocha huyo amesema kuwa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine, juzi, wachezaji
wake walionyesha kizuri lakini wakivuka, kazi itakuwa ngumu zaidi.
Pluijm
alisema wapinzani wao Al Ahly, watakaocheza baada ya kuvuka dhidi ya Komorozine ya Comoro ni wazuri na wazoefu.
“Tumefanya
vizuri mechi ya kwanza tukiwa nyumbani, japo bado tunatakiwa kwenda Comoro na
baada ya hapo tunakutana na Al Ahly ya Misri. Ile si timu ya kubeza kwani
naifahamu vizuri kwa sababu awali niliwahi kukutana nayo.
“Kikosi
chetu lazima tuendelee kujipanga kwa ajili ya mchezo huo kwa sababu lengo letu
kubwa ni kuhakikisha timu yetu inafika mbali katika michuano hii.
“Nguvu zetu
tunaelekeza kwenye mchezo uliopo mbele yetu. Lazima tuhakikishe tunajiandaa
vyema,” alisisitiza.







0 COMMENTS:
Post a Comment