Nani alikuwa vibaka wa power window wanaokera watu hasa hapa
nchini wako jijini Dar tu. Sikiliza hii kutoka nchini Ujerumani.
Vibaka wamemliza mshambuliaji nyota wa Dortmund, Robert
Lewandowski baada ya kubeba tairi nne za gari lake.
Taarifa za kuondoka kwake kwamba anatarajia kujiunga na
wapinzani wao wakubwa, Bayern Munich zimeonyesha kuhusishwa na sasa atalazimika
kuingia hasara ya pauni 7,000 ili kuweka mambo sawa.
Gari hilo la kifahari aina ya Porsche Cayenne GTS lilikutwa
juu ya matofali baada ya vibaka hao ‘kutembea’ na tairi zote nne na ‘rim’ zake.
Angeweza kulipa pauni 2,000 kurekebisha mambo, lakini vibaka
wameharibu sehemu ya chini ya gari hilo, ndiyo maana analazimika kulipa zaidi
hadi pauni 7,000.










0 COMMENTS:
Post a Comment