Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
na wachezaji wa Simba, jana walijifungia kwa takribani saa nne katika makao
makuu ya klabu hiyo barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Rage aliitisha kikao hicho cha
wachezaji pamoja na benchi la ufundi kutaka kujua kilichosababisha kuboronga
mechi mbili mfululizo kwenye Ligi Kuu Bara.
Simba ilitoka sare na Mtibwa Sugar na
baadaye kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mgambo JKT, hali iliyosababisha Rage
kutaka kuzungumza nao.
Mkutano huo ulianza ulianza Saa 7:00 mchana na kumalizika saa 10 na ushee jioni na Rage alizungumza
mambo kadhaa, likiwemo suala la kutaka kujua kama wachezaji wana matatizo au
kudai.
Pamoja na wachezaji, wengine waliohudhuria
ni wajumbe wa kamati ya utendaji na SALEHJEMBE ilipata taarifa za
uhakika kuhusiana na kila kilichokuwa kinaendelea.
“Wachezaji walimtaka mwenyekiti kushughulikia
madai yao wanayoidai klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwalipa fedha zao za
mshahara kwa wakati.
“Lakini pia waligusia suala zima la
kufokewa na kocha Logarusic, Rage aliahidi kulishughulikia suala la mshahara,
lakini kuhusiana na suala la kocha alionekana kutotaka kuliingilia sana kwa
kuwa kocha pia lazima afanye kazi yake,” kilieleza chanzo.
“Lakini wachezaji pia walisisitiza
kufungwa na sare dhidi ya Mtibwa ni sehemu ya hali ya kimchezo na kuahidi
ataona katika mechi dhidi ya Mbeya City,” kilieleza zaidi chanzo.








0 COMMENTS:
Post a Comment