Timu ya
Ferroviario de Beira ya Msumbiji imekubali kazi iliyofanywa na wachezaji wawili
wa Azam, Kipre Tchetche na Salum Aboubakar ‘Sure Boy’.
Azam
ilikuwa mwenyeji wa Ferroviario kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika
uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Chamazi.
Kocha Msaidizi wa Ferroviario, Victor Martin,
alisema katika mechi hiyo hakukuwa na
mchezaji aliyeonekana uwanjani zaidi ya Tchetche na Sureboy huku akisisitiza
kuwatafutia mbinu mbadala kwa ajili ya kuwadhibiti watakaporudiana nao baada ya
wiki moja jijini Maputo, Msumbiji.
“Yaani kuna yule aliyefunga bao (Tchetche) na
aliyevaa kitambaa cha unahodha (Sure Boy), walikuwa wanacheza vizuri sana, ni
wachezaji hatari wanaohitaji ulinzi wa kutosha uwanjani lakini nafikiri
tutakaporudiana nao tutakuwa tayari tumeshapata dawa ya kuwazuia, kwa kweli ni
aina ya wachezaji ninaotamani hata siku moja tuwe nao kikosini,” alisema
Martin.







0 COMMENTS:
Post a Comment