Timu ya FerroviƔrio da Beira ya Msumbiji inatarajiwa kuwasili
nchini kati ya kesho Jumanne au Jumatano kwa ajili ya kuvaana na Azam FC katika
mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa
Chamazi, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Azam itaendelea kumkosa nyota wake John Bocco
ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akisumbuliwa na goti.
Katibu Mkuu wa Azam ,Idrissa Nassor, alisema tayari Shirikisho la
Soka Afrika (Caf), limewatumia barua likibariki mechi hiyo kupigwa kwenye
Uwanja wa Chamazi.
“Maandalizi yetu yanakwenda
vizuri, kwanza kwa upande wa ligi tunashukuru nafasi tuliyonayo ya kuongoza
msimamo, lakini tunahitaji nguvu zaidi ili tuweze kufanikiwa kuendelea kushikilia
nafasi hiyo.
“Wapinzani wetu wanatarajia
kutua nchini kati ya Jumanne na Jumatano na tutawaweka katika hoteli
zilizopitishwa na Caf ambazo ni kati ya Tansoma, Sapphire, Holiday Inn na
nyinginezo zenye hadhi.
“Bocco hatuweza kucheza mechi hiyo, badala yake atatakiwa
kupumzika ili kujiangalia zaidi kwa kuwa goti lake bado linamsumbua na
alishindwa kumudu mazoezi kwani alikuwa akijitonyesha.
“Nadhani atacheza katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo
iwapo ataendelea vizuri,” alisema Nassor.
0 COMMENTS:
Post a Comment