Mashabiki huo walikuwa hawaridhishwi na
kiwango ambacho timu yao ilikuwa inakionyesha katika mchezo huo ambao Ashanti
ilipigwa 2-0 na kuzidi kudidimiza matumaini ya kubaki ligi kuu msimu ujao.
Mashabiki hao waliokuwa uwanjani hapo,
walionekana kuwa na jazba baada ya kuona timu yao inaelemewa huku ikiwa tayari
imesharuhusu mabao mawili, ndipo walipoanza kurusha matusi na maneno ya kashfa
kwa benchi hilo la ufundi, linaloongozwa na Kibadeni.
Ashanti wanashindwa kuamini
kinachowatokea chini ya Kibadeni, hasa baada ya kuwa na matumaini makubwa baada
ya kumnasa kocha huyo mkongwe aliyeifundisha Simba katika mzunguko wa kwanza.
Ukiachana na Kibadeni, Ashanti ina
wachezaji wengine wengi wakongwe waliowahi kucheza Simba na Yanga, lakini
imekuwa haina matokeo ya kuridhisha katika mzunguko wa pili.
Tayari imeshapoteza michezo miwili
mfululizo, baada ya awali kukumbana na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment