Wawakilishi
wa Tanzania kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Young
Africans leo imeweza kufuzu raundi ya pili ya mashindano hayo kufuatia kuibuka
na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya wenyeji timu ya Komorozine de Domoni katika
mchezo uliofanyika jioni ya leo katika dimba la Uwanja wa Sheikh Said Ibrahim
Mitsamihuli.
Ikicheza mbele ya Balozi wa Tanzania nchini Comoro Bw. Chabaka
Kilumanga Young Africans imefanikiwa kufuzu hatua ya pili ya Mashindano ya
Klabu Bingwa Barani Afrika kwa jumla ya mabao 12- 2, kufutaia ushindi wa mabao
7-0 katika mchezo wa awali uliofanyika jijini Dar es salaam huku Mrisho Ngasa
akifunga "Hat-trick" katika michezo yote miwili.
Komorozine de Domoni ikicheza mbele ya Gavana wa jimbo lao la
Anjuani iliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la mapema ili kuwapa
nguvu washangiliaji wao amabo walikuja kuipa sapoti timu hiyo.
Hamis Kiiza aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 13 ya
mchezo kufuatia kuitumia vizuri krosi ya mlinzi wa kushoto Oscar Joshua
aliyepanda kuongeza nguvu mashambulizi na pasi yake kumkuta Kiiza ambaye
aliukwamisha mpira wavuni bila ajizi.
Dakika ya 22 ya mchezo, Mrisho Ngasa aliwainua mashabiki wa Young
Africans vitini kufuatia kuifungia timu yake bao la pili kufuatia migongeo
mizuri ya Haruna Niyonzima na Didier Kavumbagu.
Saimon Msuva aliipatia Young Africans bao tatu kufuatia kufanya
shambulizi langoni mwa timu ya Komorozine de Domoni baada ya pasi za viungo
Athuman idd, Haruna Niyonzima na Mrisho Ngasa kumkuta mfungaji ambaye hakufanya
makosa.
Dakika ya 41 ya mchezo makosa ya mpira ulioptezwa na Hamis Kiziza yaliwapelekea
Komorozine de Domoni kijipatia bao la kwanza baada ya mshmabuliaji wao kumtoka
Oscar Joshua na kupiga krosi iliyomkuta mfungaji.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika, Komorozine de Domoni
1 - 3 Young Africans.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Young
Africans iliwaingiza Frank Domayo, Hassan Dilunga na Said Bahanuzi waliochukua
nafasi za Athuman Idd, Saimon Msuva na Didier Kavumbagu mabadiliko ambayo
yaliongeza kasi ya mashambulizi.
Dakika ya 77 Korozine de Domoni walijipatia bao la pili kufuatia
makosa ya kiungo Hassan Dilunga baada ya mpira alipoteza kunaswa na
msahmbuliaji wa Komorozine na kuwazidi ujanja walinzi wa Young Africans na
kuukwamisha mpira wavuni.
Mrisho Ngasa aliipatia Young Africans bao la nne dakika ya 87 ya
mchezo kufuatia Said Bahanuzi kuwatoka walinzi wa Komorozine na kupiga krosi
iliyomkuta Ngasa na kuukwamisha mpira wavuni kwa kifua.
Dakika ya 90 ya mchezo Mrisho Ngasa aliendelea kuwapa furaha tena
washabiki wa Young Africans waliojitokeza uwanjani leo kuishangilia timu yao
baada ya kuipatia timu yake bao la tano na la ushindi kwa kichwa baada ya
kuitendea vyema krosi ya kiungo Haruna Niyonzima.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Komorozine de Domoni 2 - 5
Young Africans.
Mara baada ya mchezo mwamuzi wa mchezo wa leo Allister Barra
alimkabidhi mpira mshambuliaji Mrisho Ngasa kufuatia kufunga mabao 3 peke yake
(hat-trick) katika mchezo wa leo.
Baadhi ya watanzania walijitokeza kuishangilia timu yao ya Young
Africans wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Chibaka Kilumanga
walifurahishwa na ushindi huo na kusema wamefarijika na timu yao kwa
kushinda mchezo wa leo na kusema wanaitakia kila la kheri katika michezo
inayofuata.
Kesho mchana Msafara wa Young Africans umealikwa chakula cha mchana
nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro Bw.Ckibaka Kilumanaga na
siku ya jumatatu kikosi kitaanza safari ya kurejea nchini majira ya saa 6
mchana kwa shirika la ndege Precision Air.
Young Africans: 1.Dida, 2.Twite, 3.Oscar, 4.Cannavaro, 5.Yondani,
6.Chuji/Dilunga, 7.Msuva/Domayo, 8.Niyonzima, 9.Didier/Bahanuzi, 10.Ngasa,
Kiiza








0 COMMENTS:
Post a Comment