Ahadi ya kuwa Mbeya City itaitwanga
Simba leo kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya imeshindwa kutimia baada ya timu
hizo kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara
iliyopigwa kwenye Uwanja huo, Mbeya City ndiyo ilikuwa ya kwanza kuandika bao
kwa mkwaju wa penalti baada ya beki William Galas wa Simba kuunawa mpira.
Bao hilo likadumu hadi mapumziko lakini
kipindi cha pili Simba wakaonekana kupata uhai zaidi na kufanikiwa kupata bao
lililofungwa na Amissi Tambwe.
Pamoja na mashambulizi ya zamu, lakini
ilionekana Simba walikuwa wameimarika zaidi katika kipindi hicho baada ya
kubanwa sana katika kipindi cha kwanza.
Kama wangekuwa makini wangeweza
kupata bao la ushindi, lakini mwisho
mechi hiyo iliyoingiza mashabiki wengi sana ilimalizika kwa sare hiyo.
Awali, Mbeya City walikuwa wametamba
kuimaliza Simba ambayo katika mechi ya kwanza jijini Dar walitoka nayo sare ya
mabao 2-2 wenyewe wakitoka nyuma kwa mabao mawilia na kusawazisha yote.
Katika michezo yake mitatu iliyopita
ukiwemo huo wa leo, Simba imepoteza mmoja na kutoka sare miwili.







0 COMMENTS:
Post a Comment