KAVUMBAGU (KULIA) AKISHANGILIA NA WENZAKE BAADA YA KUIFUNGIA YANGA BAO DHIDI YA AZAM FC KWENYE UWANJA WA TAIFA, DAR, LEO. |
Shabiki anayeaminika ni wa Azam FC,
ameanguka na baadaye kupoteza maisha, dakika chache baada ya mshambuliaji wa
Yanga, Didier Kavumbagu kuifungia timu
yake bao.
Baada ya Kavumbagu kufunga bao hilo,
shabiki huyo aliyekuwa amevaa jezi nyeupe na kutambulishwa kwa jina la Deodatus
Isaya Mwakiangula.
Imeelezwa Mwakiangula ni meneja wa baa
ya Rose iliyo katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa madaktari viongozi waliokuwa
kwenye Uwanja wa Taifa, leo na kumhudumia Mwakiangula kabla ya kupoteza maisha,
Nassor Matuzya alithibitisha kuhusu kifo hicho.
Madaktari hao walifanya juhudi kuokoa
maisha ya MWakiangula lakini hata hivyo ilishindikana.
Kavumbagu alifunga bao lake katika
dakika ya 14, hata hivyo baadaye Azam FC walisawazisha zikiwa zimebaki dakika 8
mpira kwisha kupitia Kelvin Friday.
0 COMMENTS:
Post a Comment