March 3, 2014


Baada ya kupitia wakati mgumu hivi karibuni kutoka kwa mashabiki wa Yanga, beki wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, juzi Jumamosi aligeuka mfalme wa klabu hiyo na mashabiki kibao wakajipanga foleni kwa lengo la kupiga naye picha.


Cannavaro alipewa hadhi hiyo na mashabiki wa Yanga baada ya kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani ikiwa ni pamoja na kuifungia timu hiyo bao pekee na la ushindi katika mechi ya kimataifa ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Baada ya mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar, juzi, mashabiki wa Yanga walikusanyika nje ya uwanja huku wakimsubiri Cannavaro atoke katika vyumba vya kubadilishia nguo ili waweze kumpongeza kutokana na kazi yake kubwa ya kupambana na washambuliaji wa Al Ahly aliyoifanya uwanjani.
Mara baada ya kutoka katika chumba hicho akienda kupanda basi la timu hiyo, mashabiki hao wa Yanga walimzonga huku wikiimba nyimbo mbalimbali za kumsifia na wengine wikitaka kupiga naye picha.

Cannavaro alisema, anawaheshimu mashabiki hao na wala hana chuki nao kwani wakati ule walipokuwa wakimzomea walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kumtaka abadilike na  kurejea katika kiwango chake kama ilivyokuwa hapo zamani.

“Kwa sasa nawaomba tushikamane muda wote ili kuhakikisha tunaenda kufanya vizuri katika mechi yetu ya marudiano, yaliopita yamepita, tugange yajao,” alsema Cannavaro na kudai kuwa mechi hiyo imemwongezea heshima na rekodi kubwa katika maisha yake ya soka.


Awali, Cannavaro alikuwa akizomewa na mashabiki wa Yanga, baada ya kuonyesha kiwango kibovu katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic