Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua Watanzania Alfred Rwiza na Leslie
Liunda kusimamia mechi zake za wikiendi hii na mwezi ujao.
Liunda
ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) kati ya How Mine
ya Zimbabwe na Bayelsa United ya Nigeria itakayochezwa Jumamosi (Machi 22 mwaka
huu) jijini Bulawayo.
Waamuzi
wa mechi hiyo wanatoka Eritrea, na wanaongozwa na Maeruf Kherseed. Wasaidizi
wake ni Angeson Ogbamariam, Berhe O’Michael na Luelseghed Ghebremichael.
Naye
Rwiza atasimamia mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 20 kati ya Lesotho na Swaziland itakayochezwa kati ya Aprili 25-27 mwaka
huu jijini Maseru.
Mechi
hiyo ya marudiano itachezwa na waamuzi Duncan Lengani, Innocent Kaundula,
Hendrix Maseko na Jones Makhuwira, wote kutoka nchini Malawi.
0 COMMENTS:
Post a Comment