Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha
mshabiki Deodatus Mwakyangula kilichotokea jana (Machi 19 mwaka huu) wakati ya
mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa kwa familia ya Mwakyangula na kwetu, kwani umetokea wakati akiwa
uwanjani kushuhudia mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyomalizika kwa
sare ya bao 1-1.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Mwakyangula, na klabu ya Yanga na kuwataka
kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
0 COMMENTS:
Post a Comment