Simba imeamka baada ya kuichapa Ruvu Shooting
kwa mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Simba imekuwa ikisuasua, katika mchezo wa leo
ilipata mabao yake mawili kupitia kwa Mrundi Amissi Tambwe.
Haruna Chanongo alifunga bao la tatu kwa Simba,
lakini bado ilionekana safu yake ya ulinzi haikuwa makini sana.
Ruvu Shooting ambayo iliipa Simba presha kubwa
ilifunga mabao yake mawili kupitia kwa Said Dilunga na Jerome Lambele na nusura
wanajeshi hao wasawazishe.
Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 35
lakini katika inaendelea kubaki katika nafasi ya nne, chini ya Azam FC, Yanga
na Mbeya City.
0 COMMENTS:
Post a Comment