Atletico Madrid imezidi kujichimbia
kileleni kwenye La Liga baada ya kuichapa Getafe bao 2-0.
Lakini hofu imetawala kwenye kikosi
hicho baada ya mshambuliaji wake nyota diego Costa aliyekosa penalti na baadaye
kufunga bao katika mechi hiyo kuumia ugoko.
Costa ameumia ugoko wakati akifunga bao
hilo la pili katika dakika ya 86.
Hofu kuu ni iwapo Costa ataikosa mechi
ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea.
0 COMMENTS:
Post a Comment