Timu ya Stand United inatarajiwa
kusajili wachezaji nane kueleka Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kufanikiwa
kupanda daraja msimu huu.
Stand imefanikiwa kupanda daraja msimu huu
na kuwa muwakilishi wa Mkoa wa Shinyanga baada ya kuwafunika wapinzani wake
wakuu, Mwadui FC.
Kocha
wa Stand United, Novatus Flugence, amesema watakuwa makini katika usajili na
watasajili wachezaji nane pekee.
Novatus alisema kuwa watakuwa makini
katika suala hilo na kwamba kiwango ndiyo kitamfanya mchezaji kupewa nafasi
katika timu hiyo na siyo kuangalia ustaa.
“Katika usajili wetu kuelekea ligi kuu
tutaangalia sana suala la kiwango kwa wachezaji wetu tutakaowasajili, ambao ni nane
tu, kwani hayo ndiyo mahitaji yetu, lakini hata wale waliopo katika timu
tutaangalia zaidi uwezo.
“Tuna wachezaji wetu waliopandisha timu
lakini itatubidi kuongeza ili kuweza kukabiliana na ushindani wa ligi kuu,
maana si mdogo kama wengi wanavyofikiria,” alisema Novatus.
0 COMMENTS:
Post a Comment