April 9, 2014


Kiungo wa Yanga, Frank Domayo, ameonekana kuwa ni mtaalamu wa kupiga mikwaju ya penalti baada ya kuwadhihirishia mashabiki wa timu hiyo waliokuwepo uwanjani wakiangalia mazoezi ya timu hiyo katika Uwanja wa Boko uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar.


Yanga imekuwa ikimtumia nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kupiga penalti katika michezo tofauti huku mashabiki wengi wakiwa na maswali ya kujiuliza endapo mchezaji huyo akiwa majeruhi ni nani ataweza kulichukua jukumu hilo kikamilifu.

Majibu ya maswali yao yalipatikana jana baada ya Domayo kuonyesha ustadi wa hali ya juu katika upigaji wa penalti ambapo alimtesa kipa wake, Juma Kaseja kila mara.

SALEHJEMBE ilishuhudia wachezaji wa Yanga wakipiga penalti katika mazoezi hayo, ambapo Domayo na Cannavaro waliweza kufunga kwa ustadi wa hali ya juu huku mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo wakionekana kufurahia zaidi mabao ya kiungo huyo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic