April 9, 2014

RHINO
Pamoja na kutofanya vyema katika mechi zake za ligi kuu, timu ya Rhino Rangers imeonekana  kuingiza mapato mengi kuliko timu nyingine zinazomilikiwa na majeshi.


Rhino imefanikiwa kuingiza jumla ya shilingi milioni 26.5 ambazo ni sawa na asilimia 4.8.

Timu hiyo ambayo imefanikiwa kupanda ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu, ingawa haijaonyesha makeke mengi kama ilivyokuwa kwa wenzao Mbeya City, kwa sasa ipo katika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi.

Rhino imefanikiwa kuzishinda timu za jeshi kongwe zilizopo kwa muda katika ligi hiyo kwa kuingiza mapato mengi, ikiwa inatumia Uwanja wake wa  Ally Hassan Mwinyi Tabora, ikiwa ni timu ya sita kwa mapato hadi sasa.

Imefuatiwa na Ruvu Shooting ambayo imeingiza milioni 22.3 sawa na asilimia 4.0,  huku timu ya jeshi ya mwisho katika mapato hayo ni timu ya  Mgambo JKT ya Tanga ambayo imeingiza Sh 6,758,103.00, sawa na asilimia 1.2 ikitumia uwanja wake wa nyumbani wa Mkwakwani.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic