April 8, 2014


Real Madrid ya Hispania na Chelsea ya England zimefanikiwa kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

MADRID:
Imepoteza mchezo wa leo ikiwa ugenini kwa kufungwa 2-0, mabao yote yakiwa yamefungwa na Reus.
Lakini imeing’oa Borussia Dortmund kwa jumpa ya mabao 3-2, kwa kuwa katika mechi ya kwanza mjini Madrid, ilishinda kwa mabao 3-0.
Katika mechi ya leo, wenyeji ndiyo walionekana wana nafasi ya kushinda mabao mengi zaidi ingawa Madrid walipoteza nafasi kadhaa kupitoa Isco na Gareth Bale.
CHELSEA:
Ikiwa nyumbani, imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini na kuiondoa PSG ya Ufaransa.
Katika mechi ya leo usiku, Chelsea imeshinda kwa mabao 2-0, yakiwa yamefungwa na Andre Schurrle na Demba Ba.
Katika mechi ya kwanza, Chelsea ilipoteza kwa mabao 3-1, hivyo ilihitaji mabao mawili tu kusonga mbele.
Baada ya mechi hiyo, Kocha Jose Mourinho alionekana kuwa ni mwenye furaha kupita kiasi huku akitimua mbio utafikiri winga aliyetanguliziwa mpira.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic