Kocha Mkuu wa
Azam FC, Joseph Omog, amesema wanahitaji pointi tatu muhimu dhidi ya Ruvu
Shooting leo, ili kuweza kujihakikishia nafasi ya ubingwa msimu huu.
Azam FC inashuka
dimbani leo kumenyana na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani,
mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.
Azam inaongoza
msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 53, huku ikiwaacha mabingwa watetezi Yanga
wakiwa na pointi 49 huku zote zikiwa zimebakiza mechi tatu hadi sasa.
Omog amefunguka kuwa mechi dhidi ya Ruvu
itakuwa na umuhimu mkubwa kwao kuweza kushinda ili waweze kupata pointi tatu
muhimu zitakazowaweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.
“Ligi ni ngumu
na ina ushindani mkubwa, kila timu imejiandaa, mchezo wetu wa Jumatano utakuwa
muhimu ili kupata pointi tatu za kutupa nafasi ya ubingwa.
“Tunahitaji
kushinda ili tuweze kujihakikishia ubingwa, kila mchezaji ana ari na
tumejipanga vyema na mazoezi.
“Kila mchezaji
yupo fiti, hakuna majeruhi katika kikosi changu cha kwanza,” alisema Omog.
0 COMMENTS:
Post a Comment