Kocha Mkuu wa
Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema mchezaji Emmanuel Okwi hayupo kambini na
suala lake lipo juu ya uwezo wake na hawezi kumtumia kwenye mechi ya leo dhidi
ya Kagera Sugar.
Pluijm amesema
mbali na Okwi, kuna wachezaji wengine kadhaa hawapo, lakini yeye anaendelea
kupambana na wale waliopo.
Baada ya mchezo
wa Mgambo na Yanga jijini Tanga kuchezwa na timu hiyo kufungwa, baadhi ya
wachezaji wa timu hiyo akiwemo Emmanuel Okwi, Kelvin Yondani, Athuman Idd
‘Chuji’ na Haruna Niyonzima hawajaonekana tena uwanjani kuitumikia timu hiyo na
hata kwenye ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya JKT Ruvu hawakuwepo dimbani.
Kocha huyo alisema sababu za baadhi ya wachezaji wake
kutokuwepo kama Okwi zipo juu ya uwezo wake, hivyo hawezi kuzungumza lolote
kuhusiana na wachezaji hao lakini kwenye kikosi chake leo hawawezi kucheza.
Pluijm alisema
kuwa ataendelea kuwatumia wachezaji wake haohao waliopo kambini na si
vinginevyo kwa sababu hao ndiyo wanaofanya mazoezi na siyo ambao wapo nje ya
kambi.
“Suala la
mshambuliaji Emmanuel Okwi kutokuwepo kambini sijui ni kwa nini, sababu zipo
juu ya uwezo wangu, siwezi nikasema vitu ambavyo sivifahamu.
“Lakini kikubwa
ni kwamba mimi ninaangalia wachezaji waliopo hapa kambini, hata katika mchezo
ujao nitawatumia hawa waliopo hapa na si nje ya hapa,” alisema Pluijm.
Wakati huohuo,
daktari wa timu hiyo, Juma Sufiani, alisema kuwa, kwa sasa kikosi hicho kina
wachezaji wagonjwa wawili ambao ni Haruna Niyonzima na David Luhende ambao
walikuwa wanasumbulia na malaria lakini afya zao zimeanza kuimarika kwa kiasi
kikubwa.
“Haruna
Niyonzima na Luhende ndiyo wagonjwa lakini wanaendelea vizuri na wameanza
mazoezi mepesi binafsi kisha wataungana na timu,” alisema Juma.
0 COMMENTS:
Post a Comment