Uongozi wa Klabu
ya Simba umefunguka kuwa, iwapo Azam FC watamhitaji mshambuliaji wao Amissi
Tambwe, watakubali kuwapa lakini wabadilishane na Kipre Tchetche.
Azam ilionyesha
nia yake ya kumtaka Tambwe kufuatia uwezo anaouonyesha na kudai kuwa ipo tayari
kumsajili iwapo watakubaliana na Simba.
Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga,
amefunguka kuwa iwapo Azam wapo ‘siriazi’ kumhitaji Tambwe, basi wabadilishane
na Tchetche.
“Tutakuwa tayari
kumuachia Tambwe kwa sharti la kubadilishana wachezaji kama ilivyokuwa kwa
Abdulhalim Humud na marehemu Patrick Mafisango kwa kutupatia Tchetche.
“Sisi tupo
tayari iwapo watakuja siriazi kwani tunachoangalia ni maslahi ya timu,” alisema
Kamwaga.
Simba iliwahi
kubadilishana na Azam kwa kumtoa Humud na kupewa Mafisango ambaye alikuwa
msaada mkubwa na kuiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2011/2012.
0 COMMENTS:
Post a Comment