Na Saleh Ally
KUTOLEWA
kwa Barcelona na PSG katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,
kumetoa nafasi kwa mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, kubeba tuzo
ya mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ingawa kuna mitihani kibao kwake.
Ronaldo
anaongoza chati ya wafungaji bora wa Ulaya akiwa na mabao 14 wakati Zlatan
Ibrahimovic wa PSG mwenye 10 na Lionel Messi wa Barcelona aliyefunga nane,
hawatamfukuza tena kwa kuwa timu zao zimetolewa.
Anayeweza
kuchuana na Ronaldo ni Diego Costa wa Atletico Madrid mwenye mabao saba au
‘patna’ wake, Gareth Bale mwenye matano. Inaonyesha itakuwa aghalabu sana kwa
wawili hao kufunga zaidi ya mabao matano ili kumfikia.
Hivyo ni
wakati mwingine kwa Ronaldo kuweka rekodi mpya kwenye ufungaji bora wa Ligi ya
Mabingwa lakini pia kufikisha mara tatu kuwa mfungaji bora kwa kuwa, Messi
anaongoza kwa kushika nafasi hiyo mara nne.
Messi
alikuwa mfungaji bora katika misimu ya 2008-09, 2009-10, 2010-11, 2011-12, wakati Ronaldo akawa mfungaji bora
mara tatu katika misimu ya 2007-08, 2012-13. Iwapo Ronaldo atachukua msimu huu,
ataungana na wakali wengine waliowahi kuchukua mara tatu ambao ni Ruud van
Nisterlooy, Ferenc Puskas, Eusebio na Jean Pierre Papin.
Lakini kuna kitu kingine, kama Ronaldo atafunga bao moja
tu, atakuwa mchezaji wa kwanza kushika nafasi ya mfungaji bora wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya akiwa na zaidi ya mabao 14 ambayo imekuwa idadi ya juu kabisa.
Tokea msimu wa 1955-56, ni Jose Altafin wa AC Milan katika
msimu wa 1962-63 na Messi, msimu wa 2011-12 na Ronaldo msimu huu ndiyo
wamefanikiwa kufikisha mabao 14. Hivyo akifunga moja, ataweka rekodi mpya.
Kutokana na
mambo yanavyokwenda, inaonyesha kuwa katika mechi mbili za mwanzo, Ronaldo ana
uwezo angalau wa kufunga bao moja na kuweka rekodi hiyo mpya ya wapachika mabao
wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini kama
Madrid itavuka na kusonga mbele hadi fainali, bado Ronaldo atakuwa na nafasi ya
kufunga bao moja tena au zaidi, hivyo kuingia kwenye rekodi hiyo ambayo atapita
kwa urahisi kwa kuwa wapinzani wake wameishia njiani.
Kwa kuwa
anazidiwa na Messi kwa mara ngapi za kuwa mfungaji bora, basi naye angependa
kuweka rekodi nyingine tofauti hasa kama hiyo ya ufungaji bora wa mabao mengi
zaidi kuliko wengine wote kwa kipindi chote kwa idadi ya mabao.
WAFUNGAJI WANAOONGOZA 2013-2014
MCHEZAJI
MABAO TIMU
Cristiano Ronaldo 14 Real
Madrid
Zlatan Ibrahimovic
10 PSG
Lionel Messi 8 Barcelona
Diego Costa 7 A.
Madrid
Sergio Agüero 6 Man
City
Robert Lewandowski 6 Dortmund
Marco Reus 5 Dortmund
Gareth Bale 5 Real Madrid
WAFUNGAJI BORA KIPINDI CHOTE:
MCHEZAJI MABAO MECHI
1 Raul Gonzalez 71 142
2 Lionel
Messi 67 84
3 Cristiano
Ronaldo 64 100
4 Ruud van
Nistelrooy 56 73
5 Thierry
Henry 50 112
6 Alfredo
Di Stefano 49 58
7 Andriy
Shevchenko 48 100
8 Eusébio
46 65
9 Filippo
Inzaghi 46
81
10 Didier
Drogba 42 85
0 COMMENTS:
Post a Comment