Mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck
na kiungo Tom Cleverley wamepigwa picha wakicheza barabarani saa kadhaa baada
ya klabu yao kung’olewa na Bayern Munich katika robo fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Welbeck, 23 na Cleverley, 24, pamoja na mshikaji
wao walionekana wakijirusha na rafiki yao mwingine wa kiume pamoja na wasichana ambao hawakufahamika.
United iliwasili Manchester na wachezaji kupewa
mapumziko ya siku 10 kabla ya kuondoka kwenda Liverpool katika mechi yao ya
Premiership dhidi ya Everton, Jumapili ya Aprili 20.
Nafasi hiyo, wawili hao wakaona waitumie vizuri
kujirusha wakicheza barabarani, tena hata bila ya kuhifadhi sura zao wala woga
wowote.
0 COMMENTS:
Post a Comment