MAN CITY |
Na Saleh Ally
MOJA ya hesabu
nzuri wanazozitaka makocha wengi makini kwenye soka ni kuona timu zao zinaanza
kufunga mabao katika mechi wanazocheza.
Kawaida, timu
inapoanza kufunga inakuwa na nafasi nzuri ya kufanya vema katika mechi husika.
Kupata bao, hesabu zinakuwa nzuri zaidi na kinachofanyika ni kulilinda na
kuongeza bao jingine.
Iwapo timu
itafanikiwa kufunga bao la kwanza, halafu ikaongeza, tayari inakuwa imejiweka katika
nafasi nzuri ya kushinda mechi hiyo.
Lakini kila timu
inapoongeza bao, lazima umakini kwenye ulinzi uongezeke kwa kuwa kama
wataruhusu wapinzani kusawazisha, mara nyingi wanaosawazisha ndiyo wanaopata
nguvu zaidi, hivyo kupoteza inakuwa rahisi kwa waliofunga bao la kusawazisha..
Katika Ligi Kuu
England, timu zinazoamini au kuitumia vizuri hesabu hiyo ya kuanza kufunga
ndiyo zinazoonekana kufanya vizuri zaidi hata kwenye msimamo.
Hii inaonyesha
kiasi gani unapoanza kufunga, inakuwa kweli ni nafasi nzuri ya kufanya vyema
katika dakika 90 kwa kuwa kufunga ni sehemu ya kumchanganya mpinzani.
Liverpool ndiyo
wanaonekana kuwa wajanja wa kuwahi kufunga katika mechi zao nyingi walizocheza
wakifuatiwa na timu za Man City, Arsenal, Chelsea na Everton.
Liverpool:
Wakali hao
kutoka Anfield ndiyo wanaonekana wanaiweza zaidi kazi hiyo kwa kuwa katika
mechi 33 walizocheza za Premiership msimu huu, 25 walikuwa wa ndiyo wa kwanza
kufunga.
Katika mechi
hizo 25 walizoanza kufunga wanaonekana kuwa na wastani wa juu kwani hadi mwisho
wa dakika 90 walifanikiwa kushinda mechi 21, mbili wakatoka sare na kupoteza
mbili.
Iko hivi; yaani
zile mbili walianza kufunga, wakapoteza baada ya wapinzani wao kusawazisha na
zile mbili walianza kufunga, wapinzani wakasawazisha na kushinda.
Man City:
Katika mechi 31
za Premiership, Man City wameanza kufunga katika michezo 24 na walifanikiwa
kushinda katika mechi 20, wakipoteza mbili na kutoka sare mbili.
Utaona wastani
wa Liverpool na City hauna tofauti kubwa, pia ndiyo timu zinazopewa nafasi
kubwa kutwaa ubingwa na hii inaonyesha mpango wa kuanza kufunga unasaidia sana.
Chelsea:
Vijana wa Jose
Mourinho ni wabishi kweli, katika mechi zao 33 za ligi, 21 walianza kufunga na
wakaweka rekodi nzuri ya kushinda 18 zote walizoanza kupata bao.
Hata hivyo, nao
wakataleza, kuwa pamoja na kuanza kufunga, walishindwa kupambana na mwisho wakatoa
sare mechi mbili na kupoteza moja tu ambayo ni rekodi nzuri na inaonyesha kuwa
Chelsea wakianza kufunga ni nadra sana wapinzani kusawazisha na kupata sare au
ushindi.
Arsenal:
Ingawa wamepewa
jina kuwa ni wazee wa ‘rivasi’, lakini bado vijana wa Arsene Wenger
wanajitutumua na kutoa ushindani mkubwa kwenye Ligi Kuu England maarufu kama
Premiership.
Katika mechi 33
walizocheza, Arsenal walianza kufunga katika mechi 20 na wakaonyesha pia ni
wazuri kama wakitangulia. Kwani wamepoteza moja tu na sare moja pia.
Hivyo Arsenal ni
kati ya timu ambazo zikitangulia kufunga, ujue una kazi kubwa ya kugeuza mambo
ili kupata sare au kuwafunga.
Everton:
Msimu huu
wamezidi kuonyesha ni wazima kweli, katika mechi 32, wao wameanza kupata bao
katika mechi 18 na kati ya hizo wameshinda 16, wakatoka sare moja halikadhalika
kupoteza moja tu.
Man United:
Jamaa bado
wanajikongoja kwenye Premiership na balaa la ‘kunata’ kwenye nafasi ya saba
linaendelea kuwaandama kwa nguvu.
Ila kwenye
kuanza kufunga, wana rekodi yao nzuri tu kwamba kama wakianza kufunga bao, basi
ujue hawapotezi labda sare.
Kwani katika
mechi 33 walizocheza, wamefanikiwa kushinda 13 na mbili zilizobaki wametoa
sare, lakini hakuna timu iliyowafunga au hawajapoteza mchezo wowote baada ya
wao kuanza kufungwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment