April 14, 2014


Katika kile kilichoonekana hali ya sintofahamu, makomandoo wa Yanga, jana waliwazuia wachezaji wa timu yao kuzungumza na vyombo vya habari, huku Mrisho Ngassa ambaye alikuwa nahodha naye akikataliwa kuzungumza pia.


Tukio hilo lilitokea kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo Yanga ilikuwa ikikipiga dhidi ya JKT Oljoro katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ikipata ushindi wa mabao 2-1.

Makomandoo hao waliwazuia wachezaji wa Yanga na kuwataka kutozungumza na waandishi wa habari, huku Ngassa ambaye alikuwa nahodha naye akikataliwa kuzungumza mara baada ya kutakiwa kufanya hivyo kwa kuwa alikuwa nahodha.

“Wewe Ngassa wewe, kwani hujui kuwa mmekatazwa kuzungumza na vyombo vya habari, twende huku,” alisikika komandoo akimwambia Ngassa ambaye naye akafuata kile alichoambiwa.

Makomandoo hao waliendelea kuwakataza wachezaji wao wengine kuzungumza, lakini kiungo Simon Msuva ndiye pekee aliyezungumza na wanahabari kwa kuwa wakati anafanya hivyo makomandoo hao hawakumuona.

 SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic