Manchester City ndiyo klabu inayilipa mshahara bomba kuliko
nyingine zote duniani.
Klabu hiyo kila mwaka inamwaga pauni milioni 5.3 kwa ajili ya
mishahara ambacho ni kiwango kikubwa zaidi kulipwa.
Wastani wa mshahara kwa wachezaji wake ni pauni 102,653 kwa wiki
ambao ni wa juu zaidi.
Timu tano za Ligi Kuu England zimeingia kwenye 20 bora ya timu
zinazolipa vizuri duniani.
Liverpool ambao ni wapinzani wakubwa wa City katika kuwania
ubingwa wa England, wako katika nafasi ya 20 wakiwa na wastani wa pauni milioni
3.4 kwa mchezaji kwa mwaka.
Manchester United iko namba
nane, wastani wa pauni milioni 4.3 kwa mwaka kwa mchezaji, Chelsea wako nafasi
ya 10 kwa wastani wa takribani pauni milioni 4 kwa mchezaji kwa mwaka na
Arsenal ni namba 11 kutokana na wastani wa pauni milioni 3.9 kwa mchezaji kwa
mwaka.
0 COMMENTS:
Post a Comment