PATRICK YONDANI |
Patrick Yondani, baba mzazi wa beki wa
Yanga, Kelvin Yondani amesema mwanaye aachwe acheze mpira.
Yondani amesema mwanaye ana uwezo wa
kufanya vizuri majukumu yake kama akiaminiwa na asingependa kuona anaingizwa
matatizoni kwa mambo ya hisia.
BABA YONDANI AKIWA NA SALEH ALLY |
“Unajua kwa anayejua mpira anaweza
kujua mengi kwamba kuna kukosea na vingine. Lakini wako wasiojua na wenyewe
wanalaumu kila jambo la kwenye soka.
“Sasa wamuache Kelvin acheze mpira,
ameisharudi na ameungana na wenzake na umeona, amecheza vizuri mechi moja ile
ya Arusha.
KELVIN YONDANI AKIWA NA KASEJA |
Hivi karibuni, Yondani alishutumiwa na
mashabiki kuhusiana na kufanya uzembe hadi Yanga kufungwa bao la pili dhidi ya
Mgambo katika mechi Yanga waliyolala kwa mabao 2-1.
Baada ya hapo, beki huyo alipotelea
kusikojulikana hadi alipoibuka wakati Yanga ikiondoka jijini Dar es Salaam
kwenda Arusha kuivaa JKT Oljoro na kuishinda.
0 COMMENTS:
Post a Comment