Uongozi wa timu
ya Mbeya City, umesema utahakikisha kuwa katika michezo yao miwili iliyobaki
inaziba mianya yote ya hujuma hasa kipindi hiki ambacho vita ya ubingwa
imepamba moto.
Mbeya City
ambayo imepanda daraja msimu huu, ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46,
saba nyuma ya vinara, Azam FC.
Timu hiyo ambayo
imebakiza michezo miwili dhidi ya Mgambo JKT na Azam FC ambayo yote itachezwa
katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, imesema ni lazima ihakikishe inashinda
mechi hizo.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Kimbe alisema kwa sasa wanajipanga kupambana na hujuma
kipindi hiki ambacho wamebakiza mechi mbili pekee.
Kimbe alisema
kuwa, watahakikisha vijana wao wanapambana kwa kujituma na siyo kutumiwa na
watu ili kuweza kuihujumu timu, ingawa timu hiyo inazingatia suala la nidhamu
na maadili.
“Timu yetu kwa
sasa inafanya vitu vyake kwa tahadhari kubwa ili kuweza kuepuka hujuma na
maneno ya kashfa kipindi hiki ligi inapomalizika.
“Ingawa
tunawaamini wachezaji wetu lakini ni vizuri tukachukua tahadhari kubwa,”
alisema Kimbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment