Wakati kivumbi
cha Ligi Kuu Bara kikitarajia kufikia tamati hivi karibuni huku Azam ikiwa na
matumaini makubwa ya kunyakua ubingwa wa michuano hiyo, Kocha Mkuu wa JKT Ruvu,
Fred Felix Minziro, ametamba kuisimamisha timu hiyo katika mechi yao ya mwisho
ili kuinusuru timu yake na balaa la kushuka daraja.
JKT Ruvu hivi
sasa ipo katika hatari kubwa ya kushuka daraja, hivyo inahitaji kufanya vizuri
katika mechi zake mbili ilizobakiza kwenye ligi hiyo dhidi ya Coastal Union na Azam ili iweze kuepukana na
balaa hilo linaloinyemelea kwa hivi sasa.
Akizungumza na
Championi Jumatano, kocha huyo alisema ni vyema wakiifunga Azam kwenye mchezo
wa mwisho ili waweze kuepuka kushuka daraja.
“Tupo
katika hatari kubwa ya kushuka daraja ambayo inatukabili kwa sasa, hivyo
tunatakiwa kuwa makini zaidi ili kuepukana na hatari hiyo.
“Hata hivyo njia
pekee tuliyonayo ni kushinda mechi zetu zote mbili tulizobakiza kwa sasa dhidi
ya Coastal Union na Azam, hivyo inatubidi tujipange na kuhakikisha hatufanyi
makosa kama tuliyofanya dhidi ya Yanga,” alisema Minziro.
JKT Ruvu hivi
sasa inashika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 28 juu
ya Mgambo JKT (25), Prisons (22), Ashanti United (22), Oljoro(18) na Rhino
Rangers (16).
0 COMMENTS:
Post a Comment