April 8, 2014


Mwamuzi Antonio Miguel Mateu Lahoz, ndiye ameteuliwa kuchezesha mechi ya fainali ya Kombe la Mfalme la Hispania maarufu kama 'Copa del Rey'.

Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) limemtangaza Lahoz kuwa mwamuzi wa mechi hiyo itayowakutanisha wapinzani wakubwa Real Madrid na Barcelona.
Mechi hiyo imepangwa kupigwa Jumatano ya Aprili 16 kwenye Uwanja wa
Mestalla jijini Valencia.
Lahoz aliyezaliwa Machi 12, 1977 katika kitongoji cha Algimia de Alfara jijini Valencia anajulikana kwa kuwa mkali na asiyetaka mchezo.
Alianza kati ya uamuzi wa soka mwaka 1992 na taratibu akawa anapanda hadi mwaka 2011 alipofanikiwa kuwa mwamuzi wa kimataifa na sasa ni kati ya waamuzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic