Sangu Kamata, Arusha
Yanga imefanikiwa kuichapa JKT Oljoro kwa mabao 2-1 katika
mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Oljoro walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Jacob
Masawe katika dakika ya 67 ambaye aliwatoka mabeki Ibrahim Job na Kelvin
Yondani na kufunga.
Baada ya hapo Yanga walicharuka na kusawazisha katika dakika
ya 72 kupitia kinda Rajab Zahir aliyeingia dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Job.
Dakika mbili baadaye, Simon Msuva aliyeunganisha mpira wa
kona kuandika bao hilo.
Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 55 na kuendelea
kujichimbia katika nafasi ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment