MANJI |
Mkutano mkuu wa Yanga pamoja
utakaoambatana na uchaguzi umepangwa kufanyika Juni 5 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
klabu ya Yanga leo, imeeleza kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi Aprili
10, makao makuu ya klabu kiliazimia kuwa mkutano mkuu wa Uchaguzi wa Yanga utafanyika
tarehe hiyo.
Lakini Yanga ikaeleza kuwa, taarifa kuhusu
taratibu za uchaguzi zitatangazwa hapo baadae na Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi, Alex Mgongolwa.
Yanga sasa iko chini ya uongozi wa Yusuf Manji ambaye tayari ametangaza kutogombea tena.
0 COMMENTS:
Post a Comment