Kikosi cha wachezaji
nyota na wakongwe wa Real Madrid ya Hispania kinatarajia kutua nchini wakati
wowote kabla ya mwaka huu kwisha kucheza mechi ya kirafiki.
Kikosi hicho kitakuwa na
nyota mbalimbali kama Luis Figo, Michel Salgado, Christian Karembeu na wengine
wengi ambao watatangazwa baadaye.
RAYCO GARCIA AKIWA NA SALEH ALLY |
RAYCO GARCIA (KULIA) AKIWA NA RONALDINHO WAKATI AKIKIPIGA TIMU YA VIJANA YA BARCELONA |
Mchezaji wa zawani wa timu
za vijana za Real Madrid na Barcelona, Rayco Garcia amemuambia SALEHJEMBE kuwa
mechi hiyo itakuwa ndani ya mwaka huu kama kila kitu kitaenda vizuri.
“Nimefika hapa Dar es
Salaam kwa ajili ya kufanya maandalizi, kuangalia mazingira.
RAYCO GARCIA (KUSHOTO) AKIWA NA LIONEL MESSI |
“Lakini kuna watu maalum
ambao wanashughulikia mechi hii kufanyika hapa.
“Shirikisho la soka la
hapa, pia wana taarifa na wanajua maaendeleo ya suala hili. Hivyo tunataka
kuangalia mambo yataenda vipi,” alisema Garcia aliyekuwa ameongozana na beki wa zamani wa Simba, Talib Hilal ambaye pia ni kocha wa timu ya taifa ya ufukweni ya Oman.
Garcia ndiye alisimamia
ziara ya timu mbili za Real Madrid na Barcelona za wakongwe ambazo zilicheza
mechi ya kirafiki Muscat, Oman mwezi uliopita na Madrid kupoteza kwa mabao 2-1.
Alisema wakongwe wawili,
Zinedine Zidane na Roberto Carlos ambao ni makocha wa Real Madrid na Besiktas
ya Uturuki, hawatakuwa na nafasi ya kuja na timu hiyo nchini kama mpangilio wa
ziara hiyo utawezekana.
RAYCO GARCIA AKIWA CAMP NOU |
0 COMMENTS:
Post a Comment