Mabingwa wa soka Tanzania Azam FC wataanza kambi mpya kujiandaa msimu mpya na rasmi wataingia mapema tu, Juni
15.
Azam imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi
kwa mara ya kwanza msimu huu tangu ipande daraja ambapo imekuwa ikitoa
ushindani wa hali ya juu katika ligi kiasi cha kuzipiku timu za Simba na Yanga.
Hata hivyo, uongozi wa timu hiyo
umefunguka kuwa, usajili wa wachezaji Dider Kavumbagu, Shomari Kapombe na Frank
Domayo ndiyo utakaokamilisha usajili wa wachezaji wao msimu ujao.
Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa
Nassoro, amefunguka kuwa timu inatarajiwa kuingia kambini Juni 15, tayari
kuanza kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu huku wakiwa wameshakamilisha
usajili wote.
“Timu inatarajiwa kuingia kambini Juni
15 mwaka huu kujiandaa na ligi na kocha anatarajiwa kurudi siku chache kabla ya
kuanza kambi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya.
“Kuhusu suala la usajili, tunasajili ili
kupata wachezaji watakaotusaidia hapo baadaye na si ilimradi tu kujaza nafasi
kwa kusajili wachezaji wasio na viwango,” alisema Nassoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment