Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto ameula baada ya
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kumteua kushiriki kozi ya masuala ya
uhamisho.
Kozi hiyo ya siku mbili inaanza leo nchini Afrika Kusini
na itakuwa ni kujifunza kuhusiana na Mfumo wa Uhamisho kupitia mtandao (TMS)
ambao unaingia katika mtindo mpya zaidi.
Kizuguto amekuwa Mtanzania pekee aliyeteuliwa kushiriki
kozi hiyo nchini Afrika Kusini huku akipewa jukumu la kuwanoa wengine.
“Kweli nimepata nafasi hiyo, kawaida wanakuwa na vigezo
vyao na pia wanaangalia ulifanya uhamisho mara ngapi na kwa ufanisi kiasi gani.
“Hivyo nakwenda peke yangu kutoka Tanzania na tayari
nimeelezwa baada ya kurejea nitakuwa na jukumu la kuwanoa maofisa kutoka kwenye
klabu nyingine,” alisema Kizuguto.
Kizuguto anatarajia kurejea nchini keshokutwa Ijumaa baada
ya kozi hiyo ya uhamisho kupitia mtandao.
0 COMMENTS:
Post a Comment