KEITA (WA KWANZA KULIA AKIWA NA KIKOSI CHA SIMBA) |
Na Saleh Ally
Beki wa kati wa zamani wa Simba,
Komambil Keita ameibukia nchini Nigeria ambako sasa anacheza soka la kulipwa.
Keita ambaye aliondoka Simba baada ya
kumalizika kwa msimu wa 2012-13 amesema sasa anakipiga katika kikosi cha
Heartland cha Nigeriaakizungumza na Championi Jumatatu kutoka katika jimbo la
Imo karibu na mji wa Port Harcourt nchini Nigeria, Keita alisema mazingira ya
kazi bora zaidi.
“Ninaishi vizuri na mambo yanakwenda kwa
mpangilio zaidi ukilinganisha na ilivyokuwa Simba. Mshahara unalipwa kwa wakati
na kila kitu kinakwenda kulingana na mipango.
“Kweli hapa mambo ni mazuri lakini bado
ninakumbuka Simba kwa kuwa nina marafiki zangu wakiwemo mashabiki wa timu hiyo
ambao walikuwa ni watu wazuri sana,” alisema.
Keita ambaye amejiunga na timu hiyo
miezi nane iliyopita anasema amejihakikishia namba na kikosi chao kiliifunga
Enyimba katika mechi yao ya mwisho ya ligi.
“Hatuko vizuri sana ila sasa tunaanza
kurudi katika kipindi hiki. Ila ligi hapa ni ngumu sana kama utalinganisha na
hapo Tanzania. Unajua hapa Nigeria unaweza kucheza mechi leo na kesho ukacheza
pia.
“Wachezaji wa hapa wengi wana maumbo
makubwa na wana nguvu sana. Hivyo ninalazimika kujifua vizuri ili kuweza
kupambana,” alisema Keita.
0 COMMENTS:
Post a Comment