Hatimaye
Msajili wa Vyama vya Michezo ameyapitisha marekebisho ya katiba au rasimu ya katiba ya klabu kongwe
ya Simba.
Katika moja
ya marekebisho yaliyopitishwa na msajili huyo, cheo cha mwenyekiti kinachoshikiliwa na Ismail Aden Rage
kimefutwa na kiongozi wa juu kabisa wa Simba atajulikana kama rais.
Rage anakuwa
ndiye mwenyekiti wa mwisho katika historia ya Simba huku akiwa kati ya
wenyeviti waliofeli zaidi kutokana na mambo kwenda kombo kupita kiasi kwa
misimu miwili sasa ndani ya Simba ambayo iliambuliwa nafasi ya tatu na nne kwa
misimu miwili mfululizo.
Rasimu hiyo
ya katiba ndiyo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na baada ya zoezi hilo kumamilika
na msajili kuipitisha, sasa Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Mwenyekiti
wake, Damas Daniel Ndumbaro iko tayari kuanza kazi.
Maandalizi
ya uchaguzi ya Simba yalikuwa yanasuasua kutokana na rasimu hiyo ya katiba
kuchelewa kwa msajili.
0 COMMENTS:
Post a Comment