Kiongozi kipenzi
cha mashabiki wa Simba, Hassan Dalali maarufu kama Field Marshal leo
amemkabishi mgombea wa Urais Simba, Evans Aveva mpira.
Dalali amesema mpira huo una maana kubwa na ujumbe kwa Wanasimba na aliamua kujitokeza hadharani kwa kuwa anaamini Simba inahitaji mabadiliko.
"Huu ni wakati wa kuangalia mtu anayeweza kuisaidia klabu irudi kwenye hadhi yake. Aveva ni mtu aliyeipigania Simba kwa muda mrefu.
"Sidhani kuna haja ya kuona haya kipindi hiki kusema Aveva ni mtu sahihi na si mwingine, Simba inahitaji mabadiliko na si dharau tena," alisema mkongwe huyo.
Dalali
amemkabidhi Aveva wakati alipokuwa makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es
Salaam kurejesha fomu za ugombea urais.
Dalali
alisema aliondoka na mpira wake mara baada ya kumaliza uongozi wake kwa kuwa
alijua Simba ilikuwa inaongozwa na watu ambao si wa mpira.
Baada ya
uongozi wa Rage aliyeingia madarakani alikuwa ni Ismail Aden Rage ambaye
uongozi wake umefeli kwa kiasi kikubwa.
“Nilijua
hakuna mtu wa mpira, sasa nimeona kuna mtu wa mpira, ninayemuamini ameingia,
nimeurudisha mpira wangu,” alisema Dalali akimkabidhi Aveva mpira huo aina ya
Uhlsports.
Dalali ni
kati ya viongozi wa Simba wanaovutia zaidi mashabiki na wanachama wa timu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment