Kikosi cha Mbeya City kimepangwa katika kundi B kwenye michuano maalumu
ya Cecafa maarufu kama Nile Basin.
Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi nchini
Sudan kuanzia Mei 22 hadi Juni 2 na Mbeya City itakipiga katika Kundi B lenye
timu za El Merreikh Al Fasher ya Sudan, AFC Leopards ya Kenya na Elman kutoka
Somalia.
Michuano hiyo inayoshirikisha washindi wa pili na mabingwa wa
Kombe la FA wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na
Kati (Cecafa), Mbeya City wamepewa nafasi ya Azam FC baada ya kusema hawako
tayari.
Kundi A lina na vikosi vya El Merreikh ya
Sudan,
Victoria University (Uganda), Malakia (Sudan
Kusini) na Polisi (Zanzibar).
Kundi C ni Al Ahli Shandy (Sudan), Al Masry (Misri),
Defence (Ethiopia na Dkhill ya Djibouti.
Mwisho ni Kundi D lenye timu za Hey Al Arab ya
Sudan, Arab Contractors ya Misri, Flambeau ya Burundi na Etincelles ya Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment