May 17, 2014

STARS YENYE WACHEZAJI WENGI WA MABORESHO ILIYOCHAPWA MABAO 3-0 NA BURUNDI


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij, jana alitangaza kikosi kitakachocheza mchezo wa kesho Jumapili dhidi ya Zimbabwe, lakini akiwapiga panga nyota wote waliopatikana katika mpango wa maboresho ya timu ya taifa ulioandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Stars, inatarajia kumenyana na Zimbabwe ‘The Warriors’, katika harakati za kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, mwakani nchini Morocco, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1980 nchini Nigeria.

Nooij ambaye alichukua mikoba ya Mdenishi Kim Poulsen, katika kikosi chake kilisheheni wachezaji kutoka Azam na Yanga ambazo zimetoa zaidi ya watano katika kikosi cha majina 24.

Azam imetoa jumla ya wachezaji nane ambao ni kipa Aishi Manula, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Said Morad, Himid Mao, Hamisi Mcha, John Bocco na Kelvin Friday.

Kwa upande wa Yanga imetoa jumla ya nyota saba ambao ni kipa Deogratius Munishi ‘Dida’, Kelvin Yondan, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Simon Msuva.

Wengine (na timu zao katika mabano) ni pamoja na Jonas Mkude, Amri Kiemba na Ramadhan Singano ‘Messi’ na Harouna Chanongo (Simba), Elias Maguri (Ruvu Shooting), Shomari Kapombe (AS Cannes, Ufaransa) Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar) na Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya DR Congo wanaotarajiwa kutua leo mchana.

Aidha Nooij alisema kuwa kuwaacha wachezaji wa maboresho si kwamba amewatema jumla, ila watakuwa chini ya uangalizi kwa ajili ya kuwa hazina ya baadaye katika kikosi cha taifa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic