Aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm ambaye ameachana
na klabu hiyo baada ya kupata ofa mpya nchini Saud Arabia, juzi Alhamis
alifanikiwa kubadili historia ya klabu hiyo iliyodumu kwa zaidi ya miaka 70 na
kuandika mpya.
Pluijm alibadili historia huyo baada ya kuwa kocha wa kwanza tangu
kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1935 aliyeondoka klabuni hapo kwa kufanyiwa
sherehe iliyohudhuriwa baadhi ya
viongozi wa klabu hiyo.
Hali hiyo imeifanya Yanga imalize zama zake za kuwatimua makocha wake
wa kigeni pamoja na wale wa hapa nyumba ambao walikuwa wakiondoka klabuni hapo kwa majonzi na masikitiko
makubwa huku wakijutia uwamuzi wao wa kukubali kufindusha timu hiyo.
Makocha wengi waliowahi kuifundisha timu hiyo kabla ya Pluijm
walikuwa wakitimuliwa na wengine kuondoka hapa nchini kwa kujificha, lakini kwa
sasa jambo hilo limekuwa tofauti.
Akizungumza katika hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika makao makuu wa
klabu hiyo jijini, Dar Pluijm alisema kuwa anaondoka Yanga ila ataendelea
kuikumbuka katika maisha yake yote kutokana na mema mengi waliyomfanyia.
Alisema amieishi Ghana kwa miaka mingi lakini hakuwahi kuonyeshwa
upendo wa dhati kama alionyeshwa muda wote aliokaa Yanga, hivyo huko aendako
atakuwa barozi mzuri wa klabu hiyo.
“Nitaikumbuka sana Yanga, lakini nawaahidi kuwa nitakuwa barozi
mzuri huko niendako na tutashirikiana kwa kila jambo, nawaomba msiwe na
wasisiwasi.
“Nitahakikisha nawaletea kocha mzuri ambaye atakuwa na mapenzi ya
dhati na klabu hii kama ilivyokuwa kwangu, pia nitawaletea wachezaji wenye
kiwango kikubwa cha kucheza soka,” alisema Pluijm ambaye uongozi Yanga
umempatia jukumu la kuhakikisha anausaidia kufanya usajili.
Pluijm
alijiunga na Yanga mwishoni mwa mwaka jana kwa kusaini mkataba wa miezi sita wa
kuifundisha timu hiyo akichukua mikoba iliyoachwa na Mholanzi mwenzake Ernie
Brandts, aliyefungashiwa vilago na uongozi wa klabu hiyo baada ya kutoridhishwa
na utendaji wake kazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment